SMART SPORT YAIPELEKA TFF MAHAKAMANI BAADA YA KUSHINDWA KULIPA DENI WANALODAIWA


Wamiliki wa kampuni ya uuzaji wa vifaa vya michezo ya Smart Sport wamehuzunishwa na kauli ya Raisi wa TFF,Jamali Malinzi ya kusema kwamba haitambui kampuni hiyo kuhusiana na madai yao ya fedha ambazo kampuni hiyo inalidai shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,kiasi cha shilingi milioni 31 kutokana na mauzo ya vifaa vya michezo kwa timu za Taifa pamoja na usafiri kwa timu hizo

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Geoge Wakuganda amesema kwamba kauli hiyo ambayo ameitoa Malinzi mbele ya waandishi wa Habari si ya kiungwana na kwani kwa muda mrefu kwa pamoja wamekua wakifanya kazi kwa pamoja hivyo kauli hiyo ni sawa na kuudanganya uma wa watanzania

Aidha Wakuganda amesema kwamba awali TFF iliwapa cheki ambazo [zimebaunsi] zikashindwa kutoa fedha hivyo anashangaa na kauli hiyo ya kiongozi mkubwa wa nchi katika utendaji wa mpira wa miguu

Amesema kwamba kwa sasa akiwa na mwanasheria wake wameamua kufungua kesi katika mahakama ya Kisutu kudai madai yao kwa TFF na kesi hiyo inataraji kusikilizwa siku ya tarehe 21 ya mwezi wa saba mwaka huu

Hata hivyo amemtaka raisi huyo kuomba radhi kwa kitendo ambacho amekifanya kwani kiuhalisia kimemuhudhunisha kwa kiasi kikubwa

No comments