MBEYA CITY WAPO KAMILI KUWAKABILI TOTO AFRICANS

Kikosi cha timu ya soka ya Mbeya City,kwa sasa kinajiandaa vyema kwa ajili ya pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Toto Afrika ya jijini Mwanza,mechi inayotaraji kupigwa hapo kesho kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.

Msemaji wa wagonga nyundo wa Mbeya City,Dismas Ten,ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kwa sasa nia yao ni kuona wanapata pointi tatu muhimu,baada ya kushindwa kupata pointi hizo katika mchezo wao uliopita mbele ya Kagera Sugar.

Amesema kwamba pia amepata taarifa kutoka kwa daktari wa timu hiyo ambapo kuelekea kwenye mechi hiyo wanataraji kukosa huduma za mlinzi Haruna Shamte baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wao uliopita.

Aidha amedai kuwa mchezaji wao Mrisho Khalifan Ngasa aliyesajiliwa katika dirisha dogo la mwezi november anataraji kuwemo kwenye mechi hiyo ya kesho,baada ya kuwepo kwa dalili za kupatikana kwa ITC yake kutoka Omani.

No comments