KOCHA WA URENO KUWA KATIKA WAKATI MGUMU WA KUPANGA KIKOSI KUWAKABILI POLAND



kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ureno Fernando Santos anawakati mgumu wa kupanga kikosi chake kitakachoivaa Poland leo katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya mataifa ya Ulaya kufuatia nyota wake muhimu kukumbwa na majeruhi.
Akizungumza leo jijini Marseille kuelekea mchezo huo kocha huyo amewataja beki Raphael Guereilo na kiungo Andre Gomes ambao wapo mashakani kucheza mchezo wa leo kutokana na kushindwa kuhudhuria mazoezi tangu jumatatu.
Hata hivyo Santos amesema amekiandaa kikosi chake kwa ajili ya kushinda na kutinga nudu fainali ya michuano hiyo licha ya kukiri upinzani atakaokutana nao.

No comments