ETIENNE NDAYIRAGIJE NDIYE KOCHA MKUU WA KMC

Na,Said Ally
Uongozi wa timu ya KMC leo hii umemtangaza rasmi Etienne Ndayiragije kuwa ndiye kocha mkuu wa timu hiyo kwa ajili ya kuifundisha katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari Leo hii mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta alisema kwamba wao kama viongozi wa KMC wameamua kumpa jukumu hilo kocha Ndayiragije kwa kua wanaamini atakuza soka la vijana.

Sitta alisema kwamba lengo la klabu ya KMC ni kuendeleza soka la vijana kwa ngazi tofauti hivyo hicho ndicho kigezo ambacho wamekibaini kwa kocha huyo.

Aidha katika hatua nyingine Sitta alishindwa kuweka bayana juu ya mustakabali wa Kocha Fredrick Minziro aliyemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja baada ya kuipandisha ligi kuu.

Ndayiragije anajiunga na KMC akitokea katika klabu ya Mbao Fc ya mkoani Mwanza ambayo nayo ni miongoni mwa timu inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments