KAMISAA WA MECHI YA YANGA ASEMA MASHABIKI WATAKAOINGIA UWANJANI HAWAPASWI KUZIDI ELFU 40,LICHA YA TP MAZEMBE KUJA NA MASHABIKI 500


Mashabiki wa timu ya TP MAZEMBE,wapatao 500 wapo njiani kuja hapa nchini kwa ajili ya pambano la kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga katika mechi ambayo inataraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa kumi kamili jioni kwa saa za hapa nyumbani

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katika makao makuu ya klabu hiyo,Jerry Muro amesema kuwa mbali ya ujio wa mashabiki hao wa TP MAZEMBE pia wamepokea taarifa kutoka kwa mechi kamishina wa mechi hiyo kua mashabiki wanaopaswa kuingia kwenye pambano hilo inatakiwa wasizidi elfu 40

Amesema kwamba kwa mujibu wa taarifa yake kua endapo mashabiki watazidi kwa kiwango kikubwa basi pambano hilo litashindwa kufanyika hii inatokana na sababu ya kiusalama kwa mashabiki hao

Hata hivy Muro amewataka mashabiki wa Yanga kuwai mapemba katika pambano hilo kwani milango itaanza kuwa wazi kuanzia mishale ya saa tano za asubuhi na hakutakua na kiingilio kwenye pambano hilo huku akidai kuwa pale idadi ya mashabiki itakapotimia milango ya uwanja wa Taifa itafungwa na hakutakua na nafasi ya kuingia uwanjani


No comments