SERENGETI BOYS YAPATA USHINDI WA KISHINDO WAKIWA UGENINI


Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys imefanikiwa kusonga mbele katika harakati za kusaka tiketi kucheza fainali za Afrika kwa vijana baada ya kuibuka na ushindi wa kishindo wa mabao 6-0 wakiwa ugenini dhidi ya Shelisheli

Katika mechi ya leo, Serengeti imewaonyesha Shelisheli namana ya kucheza soka ikiwa kwao jijini Victoria kwa mabao 6-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 9-0 baada ya ushindi wa 3-0 jijini Dar es Salaam.

Hadi mapumziko, kikosi cha Serengeti Boys walikua wanaongoza kwa mabao 2-0, kabla ya kuongeza mengine manne kipindi cha pili na kuweza kuitangaza vyema Tanzania

Mabao ya Serengeti yamefungwa na Asad Ali katika dakika ta 9  na Mohammed Abdallah aliyeachia mkwaju wa nguvu katika dakika ya 43.

Kipindi cha pili walipata mabao hayo manne kupitia Hassan Juma aliyeandika bao la tatu kabla ya Issa Juma hajafunga mengine mawili na Yohanna Mkomola akamaliza kazi.

Serengeti Boys kwa sasa ni timu pekee ambayo imesalia katika mashindano kwa timu za Taifa za Tanzania hivyo kama itafanikiwa kufanya vizuri katika mechi zake mbili dhidi ya timu ya vijana ya Afrika Kusini itafuzu moja kwa moja katika michuano hiyo 

No comments