RASMI:HANS PLUIJM NDIYE KOCHA MKUU WA AZAM FC

Na,Said Ally
Klabu bingwa Afrika mashariki na kati,Azam FC,leo hii imemtangaza rasmi aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Singida United,Hans van der Pluijm kuwa ndie kocha wa klabu hiyo kuanzia sasa akirithi mikoba ya Aristica Siaoba raia wa Romania.

Msemaji wa Azam FC,Jafari Idd alisema kwamba kocha huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja na baada ya kumalizika kwa fainali ya FA itakayowakutanisha Mtibwa Sugar na Singida United,baadhi ya viongozi wa klabu hiyo watarejea na Hans jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumalizia taratibu nyingine.

Jafari alisema kwamba Hans anajiunga na Azam FC baada ya kukamirisha taratibu zote ikiwemo kuwasiliana na viongozi wa timu ya Singida United ambao ndio waliokuwa waajiri wake hapo awali.

Alisema kwamba Azam FC inaamini uwezo wa ufundishaji wa kocha huyo kutokana na mafanikio ambayo ameyapata katika baadhi vilabu ambavyo alivifundisha ikiwemo Yanga.

No comments