FELIPE SCOLARI ASEMA YUPO TAYARI KUIFUNDISHA ENGLAND



Aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari amesema yupo tayari kukifundisha kikosi cha timu ya Uingereza endapo atapata nafasi ya kufanya hivyo.
Scolari mwenye umri wa miaka 67 amesema anajua thamani ya kuwa kocha wa taifa hilo hivyo ni suala la mchakato ambao endapo utaanza na yeye atakua tayari kutwaa mikoba ya Roy Hogson.
Kocha huyo ambaye aliiongoza Brazil kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2002 aliwahi kuhusishwa na kazi hiyo mwaka 2006 siku kadhaa baada ya Sven Goran Erikson kung'atuka.
Kwa sasa Scolari amesema ataendeea kukifundisha kikosi cha Ghuanzou Evergrande ya nchini China kwa kuwa bado anamkataba nayo.
Zipo taarifa zinazodai kuwa Gareth Southgate ambaye alitajwa kua huenda akawa kocha wa muda wa Uingereza amekataa ofa hiyo kutoka kwa chama cha soka cha nchi hiyo.

No comments