YANGA WAPINGNA NA KAULI ZA JAMALI MALINZI


Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga umesema kwamba taarifa ambazo zimezungumzwa na Raisi wa TFF,Jamali Malinzi juu ya klabu hiyo kukiuka taratibu za kuingiza idadi kubwa ya mashabiki na kutakiwa kulipa tozo kwenye mamlaka ya mapato taarifa hizo kiuhalisia si za kweli

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katika makao makuu ya klabu hiyo katibu mkuu Baraka Deusidedit amesema kwamba katika kikao ambacho wamekiti na wasimamizi wa mchezo wao dhidi ya TP Mazembe,makubaliano yao ambayo yamefikiwa hayakua kama aliyoyasema Malinzi hivyo anashangaa taarifa hizo alizotoa mbele ya waandishi wa habari

Amesema kwamba hata tozo la TRA wanalosema TFF kiuhalisia kumetakiwa kusiwe na makato kwani mechi hiyo haikua na kiingilio na hata upande wao mamlaka ya mapato wamezungumza kwamba kama hakuna mapato ambayo yamepatikana wao hawatakua na jukumu la kudai makato

Aidha amesema kwamba wao kama viongozi wa Yanga yale yote ambayo yanapaswa kuyalipa watayalipa na kwa sasa wanachofanya ni kuendelea kuwasiliana na viongozi husika ili kuweza kutambua garama za ulipaji

No comments