JKT RUVU YAMPA AZIZI SALUM GILA KANDARASI YA MWAKA MMOJA


Uongozi wa timu ya JKT RUVU ya Kibaha mkoani Pwani umekamilisha usajili wa mchezaji Aziz Salum Gila ambae msimu uliopita amekua akiitumikia timu ya Mgambo JKT ya mkoani Tanga timu ambayo imeshuka daraja msimu huu

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,katibu mkuu wa klabu ya JKT RUVU, Ramadhani Madoweka amesema kwamba Gila amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kwa ajili ya kuwatumikia maafande hao

Amesema kwamba nia yao ni kusajili wachezaji sita kutokana na matakwa ya benchi la ufundi hivyo huyo atakua ni mchezaji wa pili kusajiliwa mara baada ya awali kuweza kukamilisha usajili wa Atupule Green ambae msimu uliyopita alikua anaitumikia timu ya Ndanda ya mkoani Mtwara

Madoweka amesema kwamba dhamira yao ni kuona msimu ujao wanakua na kikosi kipana ambacho kitafanya vizuri tofauti na msimu huu ambao umemalizika kwa wao kutoshindwa kufanya vyema na mwisho wake kuwa kwenye hati hati ya kushuka daraja

Aidha amesema kwamba maafande hao bado wataendelea kua chini ya kocha Abdalah Kibaden ambae ataendelea kua na jukumu la kuifundisha timu hiyo mara baada ya uongozi kuridhishwa na ufundishaji wake

No comments