OMOG ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI WA KUIFUNDISHA SIMBA


Kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog leo amesaini mkataba wa miaka mika miwili wa kuifundisha timu ya Simba katika hoteli ya Regency, Mikocheni, Dar es Salaam mbele ya Rais wa klabu, Evans Elieza Aveva 

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Aveva amesema kwamba malengo yao ni kufanya vizuri msimu ujao na njia ya kufanya vyema ni kua na benchi bora la ufundi na kua na viongozi ambao wana weledi wa kufanya mambo kwa ufasaha ya kimaendele

Mbali na kumpa kandarasi ya miaka miwili Omog pia uongozi huo umetumia fursa ya kumtambulisha rasmi Patrick Kahemela kua ndie katibu mkuu wa klabu hiyo

Aveva amesema kwamba mara baada ya kukamilisha maswala hayo kwa sasa nguvu zao wanazielekeza katika jitihada za kukiboresha kikosi cha timu hiyo ili waweze kufanya vizuri katika msimu ujao

No comments