SIMBA WAKO MBIONI KUMPA KANDARASI OMOG KWA AJILI YA KUIFUNDISHA TIMU HIYO


Kocha wa zamani wa timu ya Azam,Mcameroon Joseph Marius Omog anatarajiwa kuwasili usiku wa leo hii jijini Dar es salaam tayari kukamilisha mazungumzo ya mwisho ya kusaini mkataba wa kuifundisha timu ya Simba

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kutoka Simba zinadai kua tayari kocha huyo ametumiwa tiketi ya ndege kwa ajili ya kufika jijini Dare es salaam ambapo awali uongozi wa Simba umekua ukiwasiliana kwa njia ya simu na baadhi ya viongozi husika

Endapo mazungumzo ya kusaini mkataba yatakamili basi hiyo itakua ni mara ya pili kwa kocha huyo kuzifundisha timu za Tanzania mara baada ya awali kuwa kocha mkuu wa Azam

Omog ni moja ya makocha ambao wana sifa nzuri na mwenye taaluma kubwa ya ukocha ingawa tangu aachane na klabu ya Azam hakufanikiwa kupata timu ya kufundisha hivyo endapo kama atajiunga na Simba basi na jambo la faraja kwa upande wake

Kwa muda mrefu viongozi wa Simba wamekua wakihaha kupata kocha mkuu wa klabu hiyo ambae atakua na sifa ya kuiwezesha timu hiyo ipate mafanikio ambayo hawakuyapata kwa muda mrefu hasa kwenye ushiriki wa michuano ya kimataifa

No comments