WANACHAMA WA SIMBA WAUNGANA NA YANGA KUELEKEA KATIKA MECHI DHIDI YA TP MAZEMBE
Baadhi ya wanachama waliojitambulisha kua ni wa klabu ya Simba hii leo wameunga na uongozi wa klabu ya Yanga katika makao makuu ya klabu ya Yanga kwa lengo la kuhamasisha mashabiki wa Tanzania kwa pamoja kuiunga mkono timu hiyo ambayo inaiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu kuelekea kwenye mechi yao dhidi ya TP MAZEMBE,mechi ambayo inataraji kupigwa siku ya kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Wanachama hao wamesema kwamba wameamua kufanya hivyo kwa kuweza kutambua umuhimu wa michuano ya kimataifa hivyo ni vyema watanzania kwa pamoja wakawa wazalendo kwa kuweka utaifa mbele ksb Yanga inaiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ns kwa upande wao wataendelea kuhamasisha mashabiki wenzao wa Simba waunhane huku pia wakimtaka Raisi wa klabu hiyo Evansi Aveva nae awe mmoja katika jambo hilo la kuwaunga wapinzani wao wa jadi
Mmoja wa wanachama hao ambao wamejitambulisha kuwa ni wanachama wa Simba anaejulikana kwa jina la Risasi Mwaulanga ambae ni mwanachama wa Tawi la Sikio la Simba Kinondoni amesema kwamba wamefurahiswa na uamuzi wa uongozi wa Yanga kwa kuweza kuamua mechi hiyo mashabiki waingie bure uwanjani hivyo hilo ni jambo la faraja kwa wapenda soka hasa watu wa hali ya chini ambao wengi wao wangeshindwa kushuhudia pambano hilo
Nae mkuu wa Idara ya Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amesema kwamba katika mechi ya kesho kwa upande wao hawataangalia itikadi yeyote na amewataka mashabiki wote wajitokeze uwanjani na wanaruhusiwa kukaa mahala popote kwenye uwanja huo
Amesema kwamba kwa mashabiki wa Yanga ni vyema wakavaa jezi za timu hiyo na wale ambao sio mashabiki ni vyema wakavaa jezi za timu ya Taifa au kama kuvaa jezi yako ya klabu,hii inatokana na ushirikiano ambao wanauhitaji kwa mashabiki
Hata hivyo amesema kwamba milango ya uwanja wa Taifa itaanza kufunguliwa kuanzia mishale ya saa tano asubuhi hivyo ni vyema kila mmoja akawai mapema katika mchezo huo kwani idadi ya watu itakapotosha milango itafungwa
Post a Comment