MASHABIKI WA YANGA WATOA TAMKO KALI KWA WACHEZAJI

Wachezaji wa timu ya soka ya Yanga jana walikumbana na wakati mgumu baada ya baadhi ya mashabiki kutaka kuwapiga kwa kile kinachodaiwa wachezaji hao kucheza chini ya kiwango katika mchezo wao dhidi ya Afrika Lyon uliosha kwa timu hizo kufungana bao 1-1.

Mashabiki hao walipandwa na jazba na kulazimika kuwatolea maneno makali wachezaji baada ya mechi kuisha huku  jeshi la Polisi likifanya kazi kubwa ya kuwaondoa mashabiki hao waliozingira uzio wa uwanja wa Uhuru.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa mmoja wa wachezaji hao alipowajibu mashabiki akisema kwamba "na bado na tulipanga matokeo yawe hivyo"

Kauli hiyo haikuwafurahisha mashabiki hao kwani wengi wao walimtolea manano makali na wengine kusema kwamba mchezaji huyo hastahili kuwepo ndani ya klabu hiyo ya Yanga kwani yeye na baadhi ya wenzake si wazalendo.

Aidha wachezaji wengi walishindwa kupanda basi la timu  licha ya gari hilo kuingia ndani ya uwanja ambapo baadhi yao walitaka kupanda lakini wakashindwa baada ya mmoja wa mashabiki kuwafuata ndani na kuendelea kuwatolea maneno makali hivyo kuamua kushuka hasa baada ya kuona idaid ya mashabiki wanaongezeka.

Hata hivyo MWANDIKE.BLOGSPORT ilishuhudia wachezaji wa klabu hiyo wakipanda magali yao binafsi na wengine walisibiri kwa muda mrefu uwanjani hao ili mashabiki wapungue kwani hali ya usalama kwao haukuwa mzuri kutokana na mashabiki kutoridhishwa na matokeo hayo.

No comments