POLISI WAENDELEA KUPIGA MABOMU YA MACHOZI KUWAZUIA MASHABIKI WASIINGIE UWANJANI MARA BAADA YA UWANJA KUJAA KATIKA PAMBANO LA YANGA NA TP MAZEMBE


Jeshi la Polisi linatumia jitihada kubwa za kupiga mabomu nje ya uwanja wa Taifa kuwatawanya mashabiki mara baada ya idadi kubwa ya mashabiki kuhitaji kuingia uwanjani ilihali uwanja umeshajaa

Idadi kubwa ya mashabiki wameonekana kua na shauku ya kulitazama pambano hilo la kombe la shirikisho barani Afrika ambalo kiingilio ni bure lkn idadi ya watu ambao washaingia uwanja haiwezakani kwa mashabiki wa nje kuingia

Mashabiki hao wameonekana kupandwa na jazba na wengi wao wakikataa kuondoka hivyo sababu ikapelekea jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa ya kupiga mabomu

Aidha kwa upande wake kamisaa wa mchezo huo amesema kwamba kama hali hiyo ya kupigwa kwa mabomu nje ya uwanja na vurugu zinazoendelea kama hazitatulia basi mechi hiyo haitaweza kuchezwa

Hata hivyo jeshi la Polisi kwa kiasi kikubwa linaendelea kufanya jitihada za kutosha za kuweza kuwazuia mashabiki hao ili wasiweze kuukalibia uwanja wa taifa na zoezi hilo linaeleka kukamilika

Kwa upande mwingine aliyewai kua makamu mwenyeki wa Toto Afrika na pia mwanacha wa timu ya Yanga Waziri Gao amesema kwamba kwake amefarijika kuona idadi kubwa ya watanzania kua wanapenda soka hivyo ni jambo la faraja ambalo amelifanya mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji

Amesema kwamba vurugu ambazo zinaendelea nje ya uwanja kwa Polisi kupiga mabomu kuwazuia mashabiki zoezi hilo litafanikiwa na ana matumaini makubwa ya mechi hiyo kuchezwa kwa utulivu mkubwa

No comments