SINGIDA UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA MSHAMBULIAJI KUTOKA ZAMBIA

Na Said Ally
Timu ya Singida United imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya usiku huu kukamilisha usajili wa mchezaji Lubinda Mundia kutoka Zambia kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mundia ni mchezaji anaemudu kucheza nafasi ya ushambuliaji aliyetokea katika klabu ya Red Arrows ya Zambia.

Huyo anakuwa mchezaji wa sita kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufungwa rasmi leo hii saa sita usiku.

Mapema leo hii Singida United ilifanikiwa kuwanasa wachezaji hao ambao ni pamoja na Kambale S.Gentil (Papy Kambale) na Daniel Lyanga, pia imefanikiwa kuwanasa Ally Hamis Ng'azi,Issa Makamba,Assad Ally Juma,Mohamed Abdallah ambao hawa wote wametokea timu ya vijana ya Serengeti Boys.

ENDELEA KUSOMA MWANDIKE BLOGSPOT ITAKUJUZA MCHAKATO MZIMA WA USAJILI KWA TIMU ZOTE.

No comments