MASHABIKI WAANZA KUINGIA UWANJANI KUSHUHUDIA PAMBANO LA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA KATI YA YANGA NA TP MAZEMBE

                                           
Baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu tayari wameshaanza kuingia katika uwanja wa Taifa kushuhudia pambano la kimataifa kwa ngazi ya vilabu kati ya Yanga na TP MAZEMBE,mechi ambayo inataraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa kuanzia mishale ya saa 10:00 jioni kwa saa za hapa nyumbani

Idadi kubwa ya mashabiki wameweza kufika mapema na sasa zoezi la kuingia uwanjani linaendelea kufanyika huku idadi kubwa ya mashabiki ambao wamevalia jezi za Yanga ikionekana kua kubwa

Katika pambano hilo ambao mashabiki wanaingia bure linatarajiwa kutizamwa na watu elfu 40 kwa mujibu wa taarifa ya kamisaa wa mchezo huo hii ni kutokana hali ya kiusalama


No comments