MBAO FC MBIONI KUANZA MCHAKATO WA USAJILI WA WACHEZAJI WIKI IJAYO


Mara baada ya uongozi wa timu ya Mbao Fc ya  Ilemela mkoani Mwanza kumpa kandarasi ya mwaka moja mmoja kocha Etienne Ndiragije raia wa Burundi kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao,hii leo uongozi wa klabu hiyo umesema kwamba kwa sasa bado hawajaanza rasmi zoezi zima la usajili bali kilichopo hivi sasa ni swala zima la kocha huyo kuangalia wachezaji ambao watakaosalia kwenye timu hiyo msimu ujao

Akiongea na Saidallymwandike.blogsport,msemaji wa timu hiyo Christian Malinzi amesema kwamba zoezi la usajili wa wachezaji wapya huenda likaanza kufanyika wiki ijayo kwani lengo lao ni kuona timu hiyo inafanya vizuri kwenye ushiriki wao wa ligi kuu

Amesema kwamba kwa sasa  viongozi wa timu wamemuachia jukumu hilo kocha huyo na wao wapo tayali kuyakamilisha yale ambayo atakayoyahitaji kocha huyo hata kama atakua na nia ya kusajili mchezaji kutoka nje ya nchi


No comments