YANGA YATOA PONGEZI KWA MASHABIKI NA JESHI LA POLISI CHINI YA KAMANDA SIRO


Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga umewashukuru mashabiki,wanachama,viongozi na wachezaji wa timu hiyo sambamba na jeshi la polisi chini kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam,Saimoni Siro kwa kuweza kufanya jitihada kubwa za kuweza kufanikisha mchezo wao dhidi ya TP Mazembe unachezwa kwa hali ya utulivu

Mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amesema kwamba kama wao viongozi wamelitambua hilo hii inatokana ushirikiano mkubwa ambao umefanywa na mashabiki ambao wamejitokeza na jeshi la Polisi kudhibiti uvunjifu wa amani

Akizungumzia juu ya mechi hiyo,Muro amesema kwamba kwa upande wao wamekubaliana na matokeo hayo kwani wamefungwa kihalali ingawa wachezaji wao wamechezi kwa kiwango kikubwa katika pambano hilo lililomalizika kwa Yanga kufungwa bao 1-0

Aidha amesema kwamba mara baada ya mechi hiyo wachezaji wamepewa mapumziko ya siku mbili na watakaporejea wataendelea na maandalizi ya mechi yao inayofuata dhidi ya Medeama ya nchini Ghana

No comments