KAMATI YA MAADILI YA TFF YAPELEKE MBELE SHAURI LA JERRY MURO


Kamati ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo  Wilson Ogunde imesogeza mbele shauri la msemaji wa timu ya Yanga,Jerry Muro kutokana na kamati hiyo kushindwa kulifanyia kazi shauri hilo mara baada ya kubaini kuwepo na upungufu kwenye barua ya wito 

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari,Ogunde amesema kwamba kamati yake imeshindwa kusikiliza tuhuma zinazomkabili baada ya kuona ni kweli kumekua na mapungufu katika barua ya wito kwa sababu barua hiyo ailezi mahala ambapo Jerry Muro anaitwa katika kamati gani ya TFF

Amesema kwamba kwa sasa kama wao kamati ya maadili wameiagiza sekretaliet ya TFF kuhakikisha kwamba Muro anapewa wito mwingine ambao utapangwa siku ya kusikilizwa pia afahamishwe kua anaitwa na kamati gani

No comments