NEYMAR DA SILVA YUKO MBIONI KUONGEZA MKATABA MPYA


Mshambuliaji matata wa mabingwa wa La Liga Fc Barcelona Neymar da Silva Santos JĂșnior yupo mbioni kusaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaorefusha ule wa awali kwa miaka mitano zaidi.

Rais wa wacataluna hao Mario Bartomeo amesema kuwa ndani ya siku chache zijazo watatangaza juu ya kukamilika kwa zoezi hilo huku akusisitiza kuwa Neymar hataki kuondoka klabuni hapo licha ya uwepo wa tetesi za kuwaniwa na klabu kubwa Barani Ulaya.

Tangu atue klabuni hapo mwaka 2013 akitokea Santos ya Brazil Neymar amekua na mafanikio makubwa ambapo msimu uliopita amefunga mabao 31 katika mechi 49 alizocheza.

Mbali na Neymar rais huyo amesema wanatarajia kurefusha mkataba na nyota wao wengine Lionel Messi na na Javier Mascherano ambao wote mikataba yao inamalizika mwaka 2018

 Bartomeu amesema wanahitaji kuongeza mapato ya klabu ili waweze kuendelea kuhodhi wachezaji wao bora kama ilivyo sasa ambapo kwa mujibu wa mwaka wa mwisho wa kifedha klabu yao imevuna kiasi cha euro 670 huku ikifanikiwa kupunguza deni lao kwa euro milioni 40.

No comments