THOMASI ULIMWENGU AWAPONGEZA YANGA LICHA YA KUFUNGWA WAKIWA NYUMBANI

 
Mchezaji wa timu ya TP Mazembe raia wa nchini Tanzania Thomas Ulimwengu amesema kwamba kwa upande wao wamefurahishwa na matokeo ambayo wameyapata ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mechi ambayo imechezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
Ulimwengu amesema kwamba dhamira yao ilikua ni kupata ushindi katika mechi hii na ndio maana wameamua kutumia mfumo wa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza
Amesema Yanga ni timu nzuri na wamecheza soka la ushindani hivyo nao wanastahili kupongezwa licha ya kufungwa wakiwa nyumbani

No comments