BAADA YA KUONDOSHWA KATIKA MICHUANO YA EURO 2016 KOCHA WA UINGEREZA ABWAGA MANYANGA
Saa chache tu baada ya timu ya
kandanda ya Uingereza kubanduliwa nje ya mashindano ya mwaka huu ya Euro
2016, Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu wadhfa wake.
Hodgson alikuwa ameshuhudiwa uingereza ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Iceland katika mkumbo wa 16 bora huko ufransa.Kocha huyo mwenye umri wamiak 68 amekiongoza kikosi hicho cha Uingereza kwa miaka 4 sasa.
Hodgson alichukuwa wadhfa huo kutoka kwa kocha muitaliano Fabio Capello aliyetimuliwa kufuatia matokeo duni.
Hata hivyo kocha huyo hajakuwa na wakati mzuri kileleni mwa Uingereza, Hodgson ameiongoza Uingereza kushinda mechi tatu tu kati ya 11 alizoshiriki katika michuano mikubwa ya dunia .
Lakini kitumbua chake kiliingia mchanga baada ya Iceland - yenye jumla ya watu 330,000 - na moja kati ya timu za mataifa yaliyoorodheshwa ya chini kabisa katika orodha ya FIFA ilipoinyuka Ui
Iceland inaorodheshwa katika nafasi ya 34.
''niwieni radhi kuwa uongozi wangu wa timu hii umekomea hapo na kwa njia hii, lakini vitu kama hivi hutokea'' alisema Hodgson .
''Vijana wamejikakamua na wamefanya kila kitu nilichowataka.
''Natumai tutashuhudia timu hii ikifuzu kwenye fainali angalu moja hivi karibuni'' aliongezea kocha huyo kwa huzuni.
ngereza.
Tangu atwae uongozi wa timu hiyo Hodgson, Uingereza imeshinda mehi 33 kati ya 56 .
Kocha huyo aliwahi kuifunza Liverpool na West Brom
Post a Comment