YANGA YAKATAA KUWALIPA TFF NA DRFA BAADA YA MECHI YA JANA DHIDI YA TP MAZEMBE,


Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limesema kwamba uharibifu ambao umefanyika katika uwanja wa Taifa wanaopaswa kulipa ni timu ya Yanga ambao wao ndio wahusika wa mchezo huo

Ofsa Habari wa TFF,Alfred lucas amesema kwamba kwa sasa uongozi husika wa uwanja huo unaendelea kufanya tasmini ya gharama zinazopaswa kulipwa mara baada baadhi ya vifaa vya uwanja huo kuhalibiwa na mashabiki ikiwemo kuvunjwa kwa geti la kuingilia

Amesema kwamba mbali na hilo pia Yanga wanafahamu kua wanahitajika kulipa gharama cha mchezo na mambo mengine ambayo hua yanafanyika katika mechi ambazo zinachezwa uwanjani hapo

Wakati huo huo uongozi wa Yanga umesema kwamba kwa upande wao wanachopaswa kulipa ni gharama husika ambazo zinapaswa kulipwa ikiwemo juu ya kukodi uwanja na gharama za jeshi la Polisi kwa kua maswala hayo yapo mikononi mwao lakini grama nyingine kama mgawo wa TFF,DRFA na mengine hayo hawatayafanya

Mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amesema kwamba mechi ya jana dhidi ya TP Mazembe haikua na kiingilio hivyo hakutakua na garama zozote za kulipa zaidi ya hizo walizosema

No comments