STEND UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA WACHEZAJI 15 AKIWEMO MCAMEROON YUSUPH SABO

                              KATIBU MKUU WA STEND UNITED JONAS TIBOROHA
Uongozi wa timu ya Stend United ya mkoani Shinyanga umetangaza rasmi kukamilisha usajili wa wachezaji 15 ambao msimu ujao wanataraji kuitumikia timu hiyo katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara

Msemaji wa timu hiyo,Alexnder Sanga amesema kwamba miongoni mwa wachezaji hao  wapo baadhi ya wachezaji wa kigeni akiwemo Yusuph Sabo ambapo msimu uliopita alikua kunako klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga pamoja na Jerome Stima aliyesajiliwa kutoka Lyon Sport ya Rwanda

Aidha amedai kua pia wamefanikiwa kumuongezea Abuu Ubwa mkataba wa miaka miwili ili aweze kuendelea kuitumikia timu hiyo msimu ujao

Hata hivyo amesema kwamba leo hii wamekamilisha usajili wa beki namba tano wa Afrika Sport ya mkoani Tanga Hussein Hamili kwa mkataba wa miaka miwili

Aidha ungozi huo umeachana rasmi na kocha Patrick Liewig kutokana sababu ya kutorizishwa na ufundishaji wake kwani nia yao msimu ujao ni kuweza kufanya vizuri katika michezo mbalimbali

Hata hivyo kuanzia sasa wakati wowote uongozi wa klbu hiyo utamtangaza kocha mpya ambae ataanza kukiandaa kikosi hicho kinachotaraji kuanza kufanya mazoezi siku ya jumamosi jijini Dar es salaam.

No comments