AYUBU NYENZI NA WENZAKE WATINGA TFF WAKIPINGANA NA MAAMUZI YA MKUTANO MKUU WA YANGA



Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limepokea malalamiko kutoka kwa wanacha na viongozi wa klabu hiyo wakipinga maamuzi ambayo yamefikiwa kwenye mkutano mkuu wa dharura wa klabu na kufikia maamuzi ya kuwaondoa baadhi ya viongozi wa klabu hiyo

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Ofsa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kwamba wanachama hao ambao wamewasilisha malalamiko ya kupinga maamuzi ya mkutano mkuu wa zarura ni pamoja na Ayubu Nyenzi,Hashim Abdalah na Salum Mkemi

Lucas amesema kwamba wanacha hao kwa pamoja wanapingana maamuzi hayo ya kuwaengua kwenye nafasi ya ujumbe kwani maamuzi hayo hayakufuata katiba halali ya klabu

Amesema kwamba kwa upande wa TFF,wamepokea malalamiko hayo na kilicho ni kamati husika kukaa na kujadili swala ili kulitolea ufafanuzi wa kina kwa kufuata taratibu na sharia zilizopo.

No comments