TAMBWE AREJESHWA DAR

Na,Said Ally,Zanzibar
Mshambuliaji Amissi Tambwe mchana huu amelazimika kuondoka kambini mjini Zanzibar kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia kusumbuliwa na homa.

"Ana malaria,kwa siku zaidi ya nne sasa amekuwa na wakati mgumu, tumelazimika kumrejesha Dar ili apate matibabu zaidi" -alisema  Dr Bavu.

Kwa upande wake kocha msaidizi wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa alisema kwamba,kikosi chake kipo kamili kuwavaa Singida United katika mchezo wao wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea kufanyika hapa Zanzibar.

Nsajigwa alisema kwamba Yanga ina wachezaji wengi hivyo anaamini yoyote atakaepata nafasi katika mchezo huo utakaochezwa kunako mishale ya saa mbili na robo ataweza kuisadia vyema timu hiyo.

Yanga na Singida United zinataraji kuingia katika mchezo huo huku timu zote zikifanikiwa kufuzu nusu fainali katika kundi B,ambapo mchezo huo utatoa mshindi atakaeongoza kundi hilo lililokuwa na timu sita.


No comments