MENEJA WA MOHAMED HUSSEIN "TSHABALALA AWEKA BAYANA TAARIFA ZA MCHEZAJI HUYO JUU YA KUJIUNGA NA YANGA


Meneja wa mchezaji wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’,Henry Mzozo amesema kwamba mchezaji huyo ataendelea kusalia kunako klabu ya Simba licha ya kuwepo na taarifa kwamba beki huyo anawindwa na Yanga kwa ajili ya kukamilisha usajili wake

Mzozo amesema kwamba  Tshabalala anaetarajiwa msimu ujao kujulikana kama Zimbwe Jr bado amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Simba na bado viongozi wa timu hiyo wana nia ya kuendelea kua nae kwa kumpa mkataba mpya hivyo anashangaa taarifa hizo ambazo zimezagaa sehemu mbalimbali kwa kuhisishwa kusajiliwa na Yanga

Aidha amevitaka vilabu ambavyo vinamuhitaji kuweza kwenda kuzungumza na viongozi wake kwani wao ndio wenye mamlaka zaidi kwa sasa

Hata hivyo amesema kutokana na kiwango bora ambacho amekionyesha mchezaji huyo kwa msimu huu ndio kimekua kikwazo cha idadi kubwa ya timu kuhitaji huduma yake

No comments