UJIO WA EMMANUEL OKWI WAOTA MBAWA

Wakati mashabiki wa timu ya soka ya Simba wakiwa na shauku ya kumuona Emmanuel Okwi akiwasili leo hii kwa ajili ya kuja kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo,uongozi wa Simba umesema kwamba mchezaji huyo kwa siku ya leo hatoweza kuwasili hapa nchini kama inavyoelezwa.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba,Said Tully ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba Okwi hatowasili kwa siku ya leo kutokana na baadhi ya mambo kutokamilika hivyo wanachama wanatakiwa kutambua swala hilo.

Alisema kwamba uongozi utawapa taarifa rasmi siku atakayowasili mchezaji huyo,hivyo ni vyema wakafuatilie maelezo ya taarifa za klabu na kuachana na habari za mitandaoni.

No comments