YANGA WATAMBA KUIFUNGA SIMBA

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Simba hapo kesho katika mchezo wa Ngao ya jamii utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa 11 jioni.

Afsa Habari wa Timu hiyo,Dismas Ten ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba tayari kikosi kimesharejea jijini Dar es salaam kikitokea Pemba kilipokwenda kuweka kambi ya maandalizi ya kujiwinda na mchezo huo.

Dismas amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi hapo kesho ili kuwapa hamasa wachezaji kuhakikisha timu inaibuka na ushindi wa kishindo.

No comments