SIMBA YATANGAZA MENEJA MPYA

Uongozi wa klabu ya Simba umefanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi la klabu hiyo baada ya kumtangaza Richard Robert kua ndie meneja wa timu hiyo ya Simba.

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano ndani ya klabu ya Simba,Haji Manara alisema kwamba Richard anachukua nafasi ya doctor Kapinga aliyerejea kwa mwajili wake ili kuendelea na shughuli zake za awali ambae kitaaluma ni dakitari wa binadamu.

Manara alisema kwamba Richard ni miongoni mwa wadau wakubwa wa mchezo wa soka na ana uzoefu wa maswala ya michezo ambae aliwai kufanya kazi na kampuni mbalimbali ikiwemo kituo cha kukuza vipaji cha michezo cha Jakaya Kikwete.

No comments