MAYANJA AAMUA KUACHANA NA SIMBA

Kocha Jackson Mayanja ameachana rasmi na klabu ya Simba baada ya kueleza kua matatizo ya kifamilia ndiyo yaliyomfanya aachane na klabu hiyo.

Mayanja alisema kwamba matatizo ya kifamilia ndio yaliyomfanya aondoke katika klabu hiyo ya Simba na hakuna jambo lolote zaidi ya hilo.

"Kwanza nawashukuru mashabiki wa Simba na uongozi wa Simba,mimi tatizo ninalo ni la kifamilia nimetoka Kampla nikarudi hapa nikawaambia niko na tatizo na la kifamilia,sasa vitu vyote vinavyoendelea vinavyoeleza nimefukuzwa hivo sivijui"alisema Mayanja.

Aidha Mayana alisema kwamba licha ya kuondoka kwake ndani ya klabu ya Simba lakini ana imani Simba itakua bingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara kwani wana kikosi kizuri.

No comments