MTIBWA SUKARI KUIVAA YANGA JUMAPILI

Kikosi cha Mtibwa Sugar Sports Club jana kililazimishwa sare ya bila kufungana na Maji maji Fc ya mjini Songea Ruvuma katika mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League)

Baada ya mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Majimaji Songea Mtibwa Sugar Sc imefanikiwa kukusanya pointi 34 na kuendelea kuwa katika nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu bara.
Kikosi hicho cha wana tam tam kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki leo mjini Mbinga kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Yanga tarehe 13.

Mchezo unaofuata wa wana tam tam utakuwa dhidi ya Yanga na mchezo huo utachezwa Jumapili 13/05/2018 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro .

No comments