YANGA WATANGAZA KUMPOKEA MANJI KWA MIKONO MIWILI

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba unamkaribisha kwa mikono miwili aliyekuwa mwenyikiti wa klabu hiyo Yusuph Manji kurejea klabuni ili kuendelea na majukumu ya kiutendaji ndani ya klabu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba endapo kama Manji ataamua kurejea ndani ya klabu ya Yanga kwao kama uongozi hawana shida kwani nafasi yake ya uwenyekiti wa klabu bado iko wazi.

Alisema kwamba Manji alitangaza kujiuzulu ndani ya klabu hiyo lakini kamati ya utendaji na wanachama bado hawajakubaliana na maamuzi yake hivyo bado majadiliano ya swala hilo yanaendelea na wanachama wataamua katika mkutano mkuu wa klabu.

No comments