MWAISABULA AWAONDOA HOFU WANA YANGA

Mchambuzi wa mpira wa miguu hapa nchini pia akiwa kocha wa mchezo huo, Kennedy Mwaisabula amesema kwamba mchezaji Haruna Niyonzima ameondoka katika klabu ya Yanga wakati mzuri ambao utawafanya viongozi kufanya usajili utakaoziba pengo lake.

Mwaisabula alisema kwamba Yanga ina nafasi ya kupata mchezaji atakaeziba pengo lake kama watajikita kufanya usajili mzuri sehemu mbalimbali ikiwemo hata hapa nchini kwani Tanzania kuna wachezaji wengi ambao wakipewa nafasi wanao uwezo wa kufanya vizuri.

Hata hivyo alisema kwamba Niyonzima ni mchezaji mzuri ambae ameipa mafanikio makubwa Yanga tangu alipojiunga na klabu hiyo hivyo anastahili kuheshimika kwa mchango wake alioutoa klabuni.

No comments