TSA WAWAPONGEZA WADHAMINI

Uongozi wa chama cha mchezo wa kuogolea hapa nchini TSA umewashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kuidhamini timu ya Taifa ya mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya dunia yanayotaraji kufanyika Budapest nchini Hungary mwezi wa nane mwaka huu.

Katibu mkuu wa chama cha kuogelea Tanzania TSA,Ramadhani Namkoveka alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi wa chama hicho unawashukuru wadhamini hao huku pia akiwataka wadau wengine wajitokeze kuisapoti timu hiyo ya taifa ili ifanikiwe kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ya dunia.

No comments