MTIBWA SUGAR WAMJAZA UPEPO SHABANI KADO

Baada ya kukamilisha usajili wa mlinda mlango Shabani Kado,uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umesema kwamba mchezaji huyo atakuwa msada mkubwa katika timu.

Msemaji wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru alisema kwamba anaamini kurejea kwa Shabani Kado ndani ya Mtibwa Sugar kutakuwa na tija kubwa kwa klabu na mchezaji mwenyewe.

Kifaru alisema kwamba Kado bado ni mlinda mlango mzuri hivyo kujiunga kwake na Mtibwa Sugar kutamfanya awe bora zaidi,kwani ndani ya timu hiyo makocha wazuri wanaomudu kutoa mafunzo bora kwa magolikipa.

No comments