KIPA BORA WA COSAFA AJIUNGA NA SIMBA

Mlinda mlango mahili wa timu ya Mtibwa Sugar pamoja na timu ya Taifa,Said Mohamed amejiunga rasmi na klabu ya Simba,baada ya klabu hiyo kumpa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia wekundu hao wenye makazi yao mitaa ya Msimbazi K/Koo jijini Dar es salaam.

Said Mohamed ambae ni chaguo la pili la kocha Salum Mayanga anajiunga na Simba ambapo huko nako anataraji kukutana na Aishi Manula ambae ndie chaguo la kwanza la Mayanga katika kikosi cha timu ya Taifa.

Said Mohamed ni moja ya wachezaji wa timu ya Taifa ambao katika michuano hiyo alinyakuwa tuzo ya kipa bora.

No comments