KASEKE AISHUHUDIA SINGIDA UNITED IKITOA KIPIGO KWA ALLIANCE

Timu ya soka ya Singida united imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga timu ya soka ya Alliance kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mabao ya Singida united yalifungwa na Elisha Muroiwa katika dk ya 10 na bao la pili lilifungwa na Tafasdwa Kutinyu kwa mkwaju wa penati dk ya 74.

Mchezo huo ulishuhudiwa na mchezaji mpya wa Singida United,Deus Kaseke aliyesajiliwa siku ya jana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kushindwana na klabu yake ya zamani ya Yanga katika masuala ya kimaslahi.

No comments