MBWANA SAMATA AIFUNGA EVERTON

Mshambuliaji wa timu ya KRC Genk,Mbwana Samata leo hii aliendeleza rekodi yake ya kufunga katika klabu hiyo baada ya kuifungia timu yake goli la kusawazisha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton uliomalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.

Everton walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji wao mpya Wayne Rooney kunako dakika ya 45 ya mchezo.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Luminus Arena,Samata aliisawazishia Genk kunako dakika ya 55 baada ya kupiga shuti ambalo limemshinda mlinda mlango wa Everton.

No comments