SHABANI KADO ASAINI MTIBWA SUGAR

Mlinda mlango wa timu ya Mwadui Fc ya mkoani Shinyanga,Shabani Kado leo hii amejiunga rasmi na klabu ya Mtibwa Sugar baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuwatumikia wakata miwa hao wa Turiani.

Mtibwa Sugar imekamilisha usajili huo baada ya kuondokewa na kipa wao Said Mohamed ambae yeye ametimkia kunako klabu ya Simba.

Kado anajiunga na Mtibwa Sugar baada ya mkataba wake na klabu ya Mwadui kumalizika,hivyo amesaini mkataba huo akiwa mchezaji huru.

No comments