AZAM FC YATAMBULISHA WACHEZAJI SITA

Klabu bingwa Afrika Mashariki na kati,Azam fc,leo hii imewatamburisha rasmi wachezaji wake sita ambao wamewasajili kwenye dirisha dogo lililofungwa usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye michuano mbalimbali.

Zoezi hilo la utamburisho ambalo limefanyika kwenye uwanja wa Azam Complex limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu hiyo akiwemo mtendaji mkuu wa klabu Saad Kawemba pamoja na meneja mkuu Abdul Mohamed.

Wachezaji wapya waliotambulishwa ni beki Yakubu Mohammed (Aduana Stars), kiungo mkabaji Stephan Kingue Mpondo (Coton Sports), mawinga Enock Atta Agyei (Medeama), Joseph Mahundi, washambuliaji Yahaya Mohammed (Aduana Stars) na Samuel Afful (Sekondi Hasaacas).

Akizungumza wakati akitambulisha nyota hao, Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, alisema kuwa Yakubu ameingia kuziba pengo la Pascal Wawa aliyeondoka baada ya kumaliza mkataba wake huku pia Mpondo akiongeza nguvu kwenye eneo la kiungo mkabaji baada ya kuondoka kwa wachezaji wawili Michael Bolou na Jean Mugiraneza.

Alisema kuwa wengine walioingia kwenye usajili huo ni washambuliaji Afful na Yahaya ambaye ni mzoefu, wakiziba pengo la Gonazo Ya Thomas na Francisco Zekumbawira walisitishiwa mikataba yao.

Hivyo orodha ya wachezaji wapya wa kigeni wa Azam FC inayotambulika hivi sasa, ni mabeki Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu, kiungo Mpondo, kiungo mshambuliaji Agyei, washambuliaji Yahaya, Afful.

Aidha Azam FC imewatoa kwa mkopo wachezaji wake saba wa kikosi cha vijana waliojiunga na timu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), ambao ni Omary Wayne, Joshua Thawe (Friends Rangers), Rajab Odasi, Yohana Mkomola (Ashanti United), Abbas Kapombe, Godfrey Elias (Polisi Dar es Salaam) na Mohamed Sadalah (Mbeya Warriors).

Pamoja na kumrejesha beki wao wa kati, Abdallah Kheri, aliyekuwa kwa mkopo Ndanda FC kwenye mzunguko wa kwanza, piia Azam FC imempeleka kwa mkopo kwenye timu nyingine kiungo wake, Bryson Rhapael, akitoka Ndanda na kwenda Mbeya City na mshambuliaji Ame Ally akiiaacha Simba na kuelekea Kagera Sugar, huku ikiachana na winga wake, Joseph Kimwaga, ambaye ni mchezaji huru hivi sasa baada ya mkataba wake kumalizika alipokuwa Mwadui kwa mkopo.

No comments