MBAO FC YATOA DOZI KWA WAKOREA

Timu ya soka ya Mbao FC yenye maskani  yake wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza  vyema maandalizi ya ligi kuu baada ya kuifunga  timu ya Halleluyah FC kutoka nchini Korea kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mabao ya Mbao FC yalifungwa na Dickson Ambundo,James Msuva na Ndaki Robert.

Kocha mkuu wa timu ya Mbao FC, Etienne Ndairagije alisema timu yake ilicheza vyema na bado anaendelea  kujenga kikosi chake kabla ya ligi kuu kuanza  mwezi Agosti mwaka  huu.

Katika mchezo mwingine wa kirafiki timu ya Singida united imeisambaratisha  timu ya Pamba FC kwa mabao 5-0 katika uwanja mkongwe wa Nyamagana asubuhi ya leo.

Mabao ya Singida united yalifungwa na Daniel Usengimana(2),Atupele green(2) na Shafiq Batambuze(1).

No comments