KOCHA WA RWANDA ARIDHISHWA NA KIWANGO CHA MSUVA

Kocha msaidizi wa timu ya taifa Ya Rwanda Mashami Vincent amemsifu mchezaji wa Yanga pamoja na timu ya Taifa,Simon Msuva kuwa ni moja ya wachezaji wazuri anaowafahamu kutoka hapa nchini kwa muda mrefu.

Vicent alisema kwamba anamfahamu vizuri Msuva tangu akiwa kwenye ushiriki wa timu ya vijana na mara nyingi amekuwa akifanya vizuri hivyo kwake ni moja ya wachezaji ambao anakubali kiwango chake.

Alisema kwamba kwa kiwango cha Msuva anaamini atafika mbali kama ataendeleza juhudi zake za kucheza mpira.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ambao kwa muda mrefu amekuwa akiaminiwa na makocha wa timu ya Taifa pamoja na klabu yake ya Yanga.

No comments