STARS KUWAFUATA RWANDA HAPO KESHO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) hapo kesho kinataraji kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa marudiano wa kusaka tiketi ya kucheza kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya nchi (CHAN).

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba kocha mkuu Salum Mayanga ameamua kukipeleka mapema kikosi cha timu hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba huenda mchezo huo ukachezwa siku ya jumamosi badala ya jumapili kama ilivyopangwa hapo awali.

Lucas alisema kwamba kiujumla hali ya kambi ya Stars iko vizuri na kikosi hicho hadi kufikia sasa kina majeruhi wawili,Shomari Kapombe ambae anatakiwa kupumzika kwa wiki mbili baada ya kuumia katika mechi ya jumamosi pamoja na Hassani Ramadhani Kessy ambae kwa upande wake yeye inatagemea na lipoti ya madaktari kama ataweza kucheza kwenye pambano hilo.

Stars inahitaji kupata ushindi wowote au sale inayoanzia magoli mawili ili ifanikiwe kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya CHAN baada ya mechi ya awali iliyopigwa mkoani Mwanza kumalizika kwa sale ya bao 1-1.

No comments