MSUVA ABADILI SAFARI YA MOROCCO

Mchezaji wa timu ya soka ya Yanga,Simon Msuva leo hii ametarajiwa kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kwenda kuungana na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) kushiriki mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa fainali za Africa (CHAN).

Msuva alishindwa kuambatana na wenzake baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa alikuwa anahitajika na klabu ya Difaa Hassan EL Jadidi ya nchini Morocco kwa ajili ya kukamilisha zoezi la usajili wa kujiunga na klabu hiyo.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas aliiambia MWANDIKE.BLOGSPOT, kwamba awali kocha Salum Mayanga alimruhusu mchezaji huyo kwenda kumaliza taratibu hizo ambapo kulikuwepo na taarifa kwamba dirisha la usajili wa Moroco lingefungwa siku ya ijumaa.

Hata hivyo shirikisho hilo baada ya hapo lilipata taarifa kwamba dirisha la usajili nchini Moroco litafungwa agost 14 mwaka huu,hivyo TFF ikaamua ni vyema Msuva akaenda kuungana na wenzake kwani muda wa usajili bado na anaweza kuitumikia timu yake ya Taifa.

No comments