SINGIDA UNITED YATUMA SALAM KWA TIMU ZA LIGI KUU

Timu ya Singida United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla magoli 5-0 dhidi ya timu ya Pamba katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Nyamagana uliopo mkoani Mwanza leo asubuhi.

Magoli ya Singida united yaliwekwa nyavuni na mchezaji Danny Usengimana aliyepachika magoli mawili mguuni mwake pamoja na Atupele Green nae alipachika magoli mawili huku Shafik Batambuze alifanikiwa kufunga goli moja katika ushindi huo wa magoli 5-0.

Singida United iko mkoani Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kuanza mwezi ujao,hivyo ushindi huo ni kama salamu kwa vilabu vya ligi kuu ya Tanzania bara ambapo timu hiyo itashiriki.

No comments