SINGIDA UNITED WAHAMIA MKOANI DODOMA

Timu ya Singida United inataraji kuanza kuutumia uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara,baada ya uwanja wao wa Namfua kuendele kufanyiwa ukarabati.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT,Afsa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura alisema kwamba leo hii wamepokea maombi kutoka kwa uongozi wa Singida United wakihitaji kuutumia uwanja huo wa Jamhuri huku wakisubiri kukamilika kwa uwanja wao wa Namfua.

Wambura alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi wa bodi ya ligi umeridhia ombi hilo la Singida United na kilichopo kwa sasa ni kuvitaarifu vilabu ambavyo vitacheza na timu hiyo katika mechi za raundi ya kwanza kufahamu swala hilo mapema.

Aidha katika hatua nyingine Wambura alisema kwamba wiki ijayo wanataraji kupata idadi ya majina ya viwnja ambavyo vitatumika kwa ajili ya michezo ya ligi na baada ya hapo kinachofuata ni kuwaagiza wakaguzi kwenda kuviangalia kama vinafaa kutumika kwa michezo hiyo ya ligi.

No comments