CHIPUKIZI KUTOKA UGANDA AJIUNGA NA YANGA
Klabu ya Yanga imefanikiwa kumsajili mchezaji chipukizi Baruan Yahya kwa kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo ya Yanga.
Baruan aliyemaliza masomo ya kidato cha sita mwaka jana nchini Uganda amejiunga na mabingwa hao wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kupendekezwa na benchi la ufundi linaloongozwa na George Lwandamina.
Aidha kinda huyo ameikacha ofa ya kupewa uraia wa nchini Uganda ili acheze kwenye kikosi cha timu ya vijana ya taifa hilo.
Baruani ni mdogo wake na nyota wa zamani wa klabu ya Simba,Yahya Akilimali anatajwa kwamba huenda akawa mrithi wa Simon Msuva anayetarajiwa kujiunga na timu ya Difaa Hassan EL Jadidi ya nchini Morocco.

Post a Comment