KOCHA STARS AAHIDI USHINDI

Kocha msaidizi wa timu ya Tanzania'Taifa stars'ameahidi ushindi kwa timu yake kuelekea mchezo wao wa marudiano wikiendi hii na timu ya Taifa ya Rwanda katika uwanja wa stade de Kigali.

Akielezea kuhusiana na maandalizi ya Mchezo huo,kocha msaidizi wa timu hiyo Fulgence Novatus alisema timu yao imefanyia kazi mapungufu yaliojitokeza katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Rwanda ambapo walitoka  sare ya 1-1.

Novatus alisema wachezaji wote ni wazima  isipokuwa Shomari kapombe ambae aliumia  wakati wa mechi ya kwanza dhidi ya Rwanda.

Novatus alisema ana amini timu yake itaibuka na ushindi ili iweze  kufuzu na alisema mazoezi waliofanya  ana uhakika yatawapa ushindi.

Nahodha wa Taifa stars Himid  Mao amewaomba watanzania kwa ujumla waungane na kuiombea timu yao iweze  kutimiza malengo yao ya kufuzu kucheza michuano ya wachezaji wa ligi za ndani(CHAN)

No comments